Kitabu hiki kina sura saba ambazo zinaangalia sera mabali mbali kuhusu maendeleo vijijini na mchango wake kwenye kupunguza umaskini Tanzania. Kinaanza na sera zilizotungwa na kuetekelezwa kipindi cha Ujamaa na Kujijetegemea. Kina sura nyingine zinazo angalia mchango wa elimu kwenye ufanisi wa kilimo;mradi wa matrekta madogo aina ya ‘power tillers’ kwenye baadhi ya wilaya; awamu tatu za sera za ruzuku za pembejeo kwa wakulima wadogo; na kilimo cha tumbaku na hatima yake kutokana na mabadiliko kwenye soko na sera za kimataifa kuhusu zao hilo. Pia kuna sura moja inayolinganisha mbinu za ukuzaji mnyororo wa thamani kwenye zao la korosho nchini Tanzania na Vietnam na nyingine ambayo inagusia mambo muhimu ya kufanikisha ushirikiano kati ya taasisi za kiserikali na asisi zisizo za kiserikali katika kutekeleza na kufanikisha sera za kilimo nchini Tanzania.
Related Articles
Does obtaining a lot of schooling guarantee a quick transition to employment? Evidence from TVET graduates in Tanzania
This brief assesses the effect of the length of schooling on how long a Technical and Vocational Education Training (TVET) graduate spends unemployed. The analysis is motivated by observations that despite some 800,000 to 1,000,000 of graduates entering the labour market in Tanzania every year (NBS, 2015), on average the economy creates only about 250,000 […]
Tathmini ya Mfumo wa Kitaasisi wa Maboresho wa Utumishi kwa Umma
Muhtasari huu unatoa taswira fupi ya tathmini ya mchango wa ushirikishwaji wa wananchi katika mifumo badilifu ya utoaji wa huduma za maji safi na maji taka (WATSAN) nchini Tanzania. Tathmini hii imefanyika katika wakati muafaka ambapo pamoja na kuwa na zaidi ya muongo mmoja wa utekelezaji wa maboresho ya sera ya maji, machache yanafahamika kuhusu: […]
Institutional Innovations and Barriers to Competitiveness
Case Studies of Smallholder Farmers in Tanzania Tanzania’s policy path has been characterized by institutional reforms aimed at increasing efficiency and productivity in key sectors of the economy. This brief examines the potential of various forms of institutional innovations in building competitiveness of smallholder agriculture in Tanzania. Evidence used shows that while some policies and […]
Elimu na Uzalishaji Kwenye Kilimo Tanzania Vijijini
Hii ni taarifa fupi itokanayo na utafiti wa kitaalam kuhusu mchango wa mfumo rasmi na usiorasmi wa elimu, na upatikanaji wa ardhi na mikopo kwa uzalishaji kwenye kilimo Tanzania katika maeneo ya vijijini. Uchambuzi uliofanywa unasisitiza umuhimu wa elimu rasmi na ile isiyo rasmi, upatikanaji wa ardhi, na uzoefu wa muda mrefu wa stadi za […]