Muhtasari huu unatoa taswira fupi ya tathmini ya mchango wa ushirikishwaji wa wananchi katika mifumo badilifu ya utoaji wa huduma za maji safi na maji taka (WATSAN) nchini Tanzania. Tathmini hii imefanyika katika wakati muafaka ambapo pamoja na kuwa na zaidi ya muongo mmoja wa utekelezaji wa maboresho ya sera ya maji, machache yanafahamika kuhusu: Mosi, namna ambavyo wananchi wanashiriki kwenye michakato ya utengenezaji na utekelezaji wa maboresho ya huduma; na Pili: mchango ambao jamii unatoa kwenye utoaji wa huduma husika. Taswira hii inatokana na kitabu kilichojikita kwenye uchunguzi wa kina wa huduma za Maji Safi na Maji Taka uliofanyika katika kata ya Kawe, manispaa ya Kinondoni, nchini Tanzania. Utafiti ulitumia fasihi na maandishi mbali mbali kuhusu maboresho ya utumishi wa umma, ushirikishaji wa wananchi na nadharia ya kihistoria ya mfumo wa kitaasisi, katika kuwasilisha na kuchambua kwa kina utekelezaji wa dhana na sera ya ushirikishwaji wa wananchi, mahusiano kati ya watendaji wa kitaasisi na wananchi kwenye utengenezaji na utekelezaji wa maboresho ya sera utoaji wa huduma za maji safi na maji taka katika eneo la tafiti husika.
Related Articles
24th ARW Synthesizing Report
Tanzania has achieved sustained rates of economic growth for the past ten years and is moving towards middle income status. Maintaining these gains while ensuring that development is inclusive is a core objective of the second National Five-Year Development Plan which places industrialisation as the key pillar of national development strategy. Capturing value through agro-processing, […]
Tathmini ya Mfumo wa Kitaasisi wa Maboresho wa Utumishi kwa Umma
Muhtasari huu unatoa taswira fupi ya tathmini ya mchango wa ushirikishwaji wa wananchi katika mifumo badilifu ya utoaji wa huduma za maji safi na maji taka (WATSAN) nchini Tanzania. Tathmini hii imefanyika katika wakati muafaka ambapo pamoja na kuwa na zaidi ya muongo mmoja wa utekelezaji wa maboresho ya sera ya maji.
Sera za Kilimo na Jitihada za Kupunguza Umaskni Tanzania
Sera nyingi zilizobuniwa na kutekelezwa katika kipindi cha uongozi wa Baba wa Taifa wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere, zilitilia mkazo sana mendeleo vijijini kupitia sera ya Ujamaa na Kujitegemea ambayo nia yake ilikuwa ni kuondoa mifumo ambayo ilikuwa inaendeleza umaskini na dhuluma kwa walio wengi.
Does obtaining a lot of schooling guarantee a quick transition to employment? Evidence from TVET graduates in Tanzania
This brief assesses the effect of the length of schooling on how long a Technical and Vocational Education Training (TVET) graduate spends unemployed. The analysis is motivated by observations that despite some 800,000 to 1,000,000 of graduates entering the labour market in Tanzania every year (NBS, 2015), on average the economy creates only about 250,000 […]