Kuna makubaliano ya jumla kwamba marekebisho ya sera zinazohusu sekta ya kilimo, hasa katika suala la kupunguza upotevu wa mazao aina ya nafaka, yapewe kipaumbele Utafiti uliofanyika huko nyuma,ulithibitisha kwamba kiasi kinachopotea tangu kuvuna hadi kuliwa, kinafikia asilimia 40.

Upotevu huo hutegemea mazingira yaliyopo;kwa mfano: aina ya zao, mahali linapostawishwa,  na kadhalika. Hata hivyo, hakuna takwimu sahihi zinazo onyesha kiasi cha upotevu huo1 . Takwimu zinazonukuliwa ni za kipindi cha mwaka 1950 hadi 19602 . Upotevu au kuharibika kwa chakula kuna athari kubwa katika kipato na maisha ya wakulima. Kwa mfano, nafaka: Inakadiriwa kwamba kila mwaka hasara inayotokana na kuharibika kwa mazao ya nafaka barani Afrika, kusini mwa jangwa la Sahara, inafikia dola za Kimarekani bilioni 4 na hii ni sawa na asilimia 15 ya thamani ya mavuno hayo.

Read a full report attached below.

Tanzanian_Markets_PAN_-_Upotevu_wa_mazao

recommend to friends
  • Google+
  • PrintFriendly