Idadi kubwa ya Watazania huishi sehemu za vijijini, na shughuli zao kuu ni kilimo. Sekta ya kilimo hutoa ajira kwa takriban asilimia 70 ya Watanzania. Kilimo huchangia asilimia 24.6 ya Pato la Ndani la Taifa, asilimia 26 ya Mapato ya Fedha za Kigeni. Kwa kuzingatia mchango wa sekta ya kilimo katika uchumi wa taifa, mwelekeo wa jinsi sekta hii inavyotazamwa unatia wasiwasi.

Katika kipindi kati ya mwaka 2000 na 2012, wastani wa kukua kwa sekta hii ulikuwa asilimia 4.4, kiwango hiki kiko chini sana ya kile kilichowekwa na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania – MKUKUTA 1, yaani lengo la asilimia 10 ifikapo mwaka 2010. Ukuaji wa kusuasua wa sekta hii maana yake ni kuendeleza hali ya umaskini kwa idadi kubwa ya Watanzania ambao huishi vijijini. Kwa hiyo, mkakati wa kupunguza umaskini miongoni mwa Watanzania, sharti ulenge katika kuinua uchumi wa wakazi wa vijijini, mkazo mkubwa utiwe katika uzalishaji wenye tija wa mazao makuu ya chakula

Tanzanian_Markets_PAN_-_Tathmini_ya_Utimizaji

recommend to friends
  • Google+
  • PrintFriendly