Posted: Tuesday April 03, 2012 2:11 AM BT

TAASISI ya Utafiti ya Kuondoa Umaskini (REPOA), imetaja mageuzi makubwa kiuchumi na kijamii kuwa ni njia muhimu inayostahili kufuatwa katika kufanikisha vita dhidi ya umaskini Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA, Profesa Samuel Wangwe alisema hayo baada ya kongamano la 17 la mwaka la taasisi hiyo jijini Dar es Salaam akibainisha kuwa kimsingi wanasiasa wanastahili kusimamia mageuzi hayo, pamoja na kupata baraka za uongozi wa kisiasa katika nchi husika.

“Tafiti za umaskini zimethibitisha kwamba kuondoa umaskini kunataka mapinduzi makubwa ya kiuchumi na jamii, uzoefu unaonyesha kwamba mageuzi hayo yanataka kimsingi kusimamiwa na kupata baraka za uongozi wa kisiasa katika nchi husika, ” alisema Profesa Wangwe.

Alisema kuwa ingawa wataalamu wanasema kwamba uchumi wa Tanzania umekua katika miaka ya hivi karibuni, lakini bado ukuaji huo haujafanikiwa kupambana na umaskini kama ilivyotegemewa.

Akizungumzia kongamano la mwaka la REPOA lililomalizika mwishoni mwa wiki Wangwe alisema kwamba lilikuwa la manufaa kwa kuwa lilisaidia kupatikana kwa mawazo mapya yatakayofanyiwa utafiti ili kufikia mapinduzi ya kiuchumi na kijamii yanayotakiwa katika kupunguza na kumaliza umaskini nchini.

“Tumejifunza toka kwa washiriki ambao nchi zao zimeweza kufanyika kwa mabadiliko hayo na kupiga vita umaskini kwa kiwango kikubwa,” alisema.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Joseph Simbakalia aliyekuwa mmoja wa wa washiriki kongamano hilo alisema kuwa tafiti ni muhimu kwa uhai wa taifa na ni lazima zifanywe kusaidia kuleta suluhisho la matatizo ili kuweza kupata maendeleo.

Alisema hakuna iliyopata maendeleo bila ya kufanya tafiti hivyo ni lazima watafiti wafanye kazi zao kwa makini na ufanisi na kupatia majawabu waliyoyaona kwa mamlaka husika ziweze kutumia kwa manufaa ya nchi.This article was published in the Mwananchi newspaper and is also available at the following link: http://www.mwananchi.co.tz/business/13-biashara-za-kitaifa/21656-wanasiasa-wasimamie-mageuzi-ya-kiuchumi-repoa.html

http://www.repoa.or.tz/images/uploads/inthenews.png inthenews

recommend to friends
  • Google+
  • PrintFriendly