Posted: Friday May 18, 2012 2:37 AM BT

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimekosolewa kutokana na mapendekezo yake kwa serikali kama hatua za kupambana na hali ngumu ya maisha kwa wananchi.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Kitila Mkumbo, amesema anakubaliana na pendekezo la kuwataka waajili kuongeza mishahara, lakini alisema kuwa Watanzania wengi hawajaajiliwa katika mfumo rasmi.

“Kuongeza mishahara sawa, lakini isichoelewa NEC (Halmashauri Kuu ya Taifa) ya CCM ni kwamba mamilioni ya Watanzania hawajaajiriwa katika mfumo ulio rasmi na mamilioni wengine hawana ajira kabisa,” alisema na kuongeza.

“Wana uchumi wameeleza waziwazi kwamba kuna vyanzo vikubwa viwili vya kupanda kwa mfumuko wa bei nchini, ambavyo nimatumizi makubwa na mabaya ya serikali na kushuka kwa uzalisha kutokana na kutokuwa na viwanda. Mambo yote hayajagusiwa kabisa katika tamko la NEC ya CCM. Tukisema hawa bwana wapo out of touch with the realities (wako nje ya ukweli halisi wa hali za wananchi) watabisha.

Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, alisema tatizo la ugumu wa maisha la sasa CCMna serikali wasilichukulie kwa ujumlakuwa ni la sehemu kubwa ya dunia kuhalalisha udhaifu na kushindwa kwao kujenga uchumi na kodi.

“Ni kweli tatizo kubwa duniani ni chakulakutokana na mabadiliko ya ya tabia nchi kutokana na mvua duni. Hapa Tanzania uhaba wa chakula umechangia mfumuko wa bei kwa zaidi ya asilimia 60. Lakini kwa Tanzania hilo ni tatizo la kujitakia, na tungekuwa na serikali imara uhaba wa chakula kwa jirani zetu ingekuwa faida yetu kuuza nje badasla ya sasa tunaweka vizuizi,” alisema.

“Nasema hivi kwa sababu Tanzania ina jumlaya ekari milioni zinazofaa kwa umwagiliaji, 29.4 hivyo kuendelea kiathirika na mvua ni kukosa shukrani kwa Mungu. Hebu fikiria kati ya hejaru hizo zote kwa miaka 50 serikali imewekezakusaidia wakulima kulima ekari laki nne tu,” alisema na kuongeza kuwa itachukua miaka 3625 kwa serikali kuwezesha wakulima kutumia ardhi inayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji.

Alisema utafiti wa REPOA unaonyesha kwamba Tanzania ikikuza kilimo kwa asilimia 10 kwa miaka mitatu mfululizoitapunguza umaskini kwa asilimia 50. “Tangu waseme mwaka 2006 mpaka leo kilimo kinakuzwa kwa asilimia nne."

This article was published in the Nipashe newspaper and is also available at the following link: http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=41646

recommend to friends
  • Google+
  • PrintFriendly